Uhuru FM TZ
Vijana watakiwa kujitambua na kujenga falsafa chanya ya maisha
Uhuru FM TZSeptemba 2026uhurufmtz.blogspot.com
Taarifa ya Uhuru FM TZ. Washa sauti.
Vijana wametakiwa kujitambua, kufahamu uwezo wao na kusudi la maisha, pamoja na kutumia muda kwa usahihi ili kuepuka kukimbilia njia za mkato katika kutafuta mafanikio.
Wito huo umetolewa na mwandishi Amani Lyimo, wakati wa uzinduzi wa kitabu chake kinachojulikana kwa jina la “Sasa Ninajua, Falsafa 21 za Maisha”, ambacho amesema kinalenga kumsaidia kila mwanadamu kujenga falsafa yake ya maisha bila kujali dini, kabila, jinsia au utaifa.
Amesema miongoni mwa falsafa hizo ni kujifahamu, kujua kusudi la maisha, matumizi sahihi ya muda, kuwa na mtazamo chanya pamoja na uvumilivu na ustahimilivu katika kukabiliana na changamoto za maisha.
Kwa upande wake, Muidadi Mikidadi, Chief of Logistics wa Match Super Brand, amewataka vijana kujenga kujiamini na kuachana na mtazamo hasi, akisema mtazamo chanya unaweza kumsaidia kijana kuamini katika mawazo yake na kupiga hatua katika maisha.
Muidadi amesema vijana wanapaswa kuthubutu kuamini katika kile wanachokifanya na kukileta katika jamii ili kiweze kuwa na mchango kwa wengine.