Sasa Ninajua
Kutoka Kutokuelewa hadi Uelewa. Falsafa 21 za Maisha. Kitabu cha Aman Lyimo, kilichopitiwa na Prof. Anna Tibaijuka.

Kutoka Kutokuelewa hadi Uelewa
Sasa Ninajua
Falsafa 21 za Maisha
Sura ishirini na moja, kila moja ni falsafa unayoweza kuichukua na kutembea nayo. Nafuatilia kila wazo hadi mzizi wake, nalisimamisha kwa mwanafalsafa aliyeliishi, nalipima dhidi ya mkanganyiko tulionao sasa, kisha najibu swali moja: sasa nifanye nini?
Kitabu kuhusu kujenga falsafa unayoweza kuishi nayo
Watu wengi wanaishi kwa falsafa ambayo hawakuichagua. Ilitoka kwa familia, shuleni, au kwa yale ambayo umati ulikuwa unasema mwaka ule. Inafanya kazi kimya kimya nyuma ya maisha, nayo ndiyo inayoamua fedha zinavyoshikwa, kazi inavyothaminiwa na majira magumu yanavyovumiliwa.
Kwa ufupi, kila sura inatoa majibu ya nini kifanyike sasa.
Masomo yenyewe si ya nadharia tu: kazi, fedha, ustahimilivu, uhuru, mshikamano, maono, furaha. Sura ya kumi na mbili inahusu kugeuza kidogo ulichonacho kuwa utajiri bila kutegemea miujiza. Sura ya ishirini inaeleza kwa nini hakuna linalowezekana peke yako.
Maandishi haya yalihakikiwa na Askofu Bernadin Mfumbusa, na nitasema wazi: bila yeye, nisingeweza kuandika kitabu hiki.
Soma Sura ZoteKwa nini nimeandika
Falsafa ilikuwa imefungiwa seminarini
Nilisoma falsafa kwa miaka katika malezi. Kisha nikaangalia ni nani mwingine anaruhusiwa kuisoma.
Nimegundua katika maisha tunayoishi duniani sasa hivi, watu wengi wako kwenye mkanganyiko wa mambo mengi. Wanatafuta kujua ukweli wa mambo, na katikati ya hayo wanashindwa kujua kipi cha kushika na kipi cha kuacha.
Somo pekee ambalo linatoa majibu sahihi ya kitu gani tunapaswa kufanya duniani ni falsafa. Kwa bahati mbaya, katika setting ya Afrika, falsafa inafundishwa zaidi kwetu sisi mafrateri tunaokuwa mapadri. Watu wengine hawapati availability wala uwezo wa kusoma masomo ya falsafa.
Kwa hiyo baada ya kusoma falsafa miaka hiyo, niliona nije na kitabu ambacho kitawasaidia watu wa kawaida. Hasa vijana, na kila mtu anayetafuta mwelekeo na ukweli maishani, ili waweze kujua kidogo namna mambo yanavyotakiwa kwenda duniani.
Kwa maneno yangu mwenyewe. Washa sauti.
Maswali matatu
Falsafa kwa kifupi kabisa inajibu maswali makuu matatu. Hayo matatu ndiyo kitabu hiki kimejengwa juu yake.
01
Nini ni uhalisia?
What is reality?
Uhalisia wa Mungu, uhalisia wa dunia na uhalisia wa binadamu. Tuko kwenye dunia inayotuchanganya. Hatujui Mungu yupi tumfuate, kwa sababu madhehebu ni mengi, na kila siku tunasikia lingine. Na inatuchanganya pia kuhusu mwanadamu ni nini: mtu amekuwa mgumu kueleweka, anaonekana kwa namna moja na nyuma ya pazia ni mtu mwingine. Mkanganyiko.
02
Tunawezaje kujua?
How can we know?
Kujua nini: kumjua Mungu, kujua dunia na kumjua binadamu. Wengi tunatamani kujua vitu, na si kujua tu, bali kujua ukweli wa mambo. Lakini tunafikaje huko? Falsafa yenyewe ni somo la critical thinking, kwa hiyo inatusaidia kujifunza namna ya kujua vitu vizuri.
03
Tunawezaje kuishi?
How should we live?
Swali la maadili. Kila sehemu tunayoishi, iwe kwa madaktari, polisi au kanisani, kuna code of ethics. Baada ya kujua nini ni halisi na tunawezaje kujua, swali la mwisho ndilo unalopaswa kulijibu kila siku: mtu anapaswa kuishi vipi katika dunia kama hii?
PICHA
Kitabu mikononi mwa watu
Picha zote





Maoni ya Wahakiki

“Hiki ni kitabu kinachowasilisha kwa uwazi na kwa ufupi maarifa ya msingi ambayo kila kijana anapaswa kuyafahamu ili ajipange kimkakati kwa ajili ya maisha yake. Sura ya 12 inayohusu fedha ni ya kipekee kwa mafundisho yake. Vijana wanapaswa kujifunza tangu mwanzo kutambua tofauti kati ya fedha na utajiri, ili waweze kuvunja minyororo ya umaskini na hali ya kunyimwa fursa za maendeleo.”
Prof. Anna Tibaijuka
Profesa Mstaafu wa Uchumi; Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Habitat; Mbunge na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Sasa Ninajua ni kitabu kinachotia moyo na kutoa mwongozo wa vitendo kwa kufungamanisha hekima ya kudumu na changamoto za maisha ya leo. Kwa kuchanganya mafundisho ya wanafalsafa wa kale na fikra za viongozi wa kisasa wa Afrika, mwandishi amewasilisha mawazo ishirini na moja yenye maana na uwezo wa kubadili maisha.
Kitabu hiki kinawahimiza wasomaji kufikiri kwa kujitegemea, kuishi kwa kusudi na kujenga ustahimilivu, huku kikitoa mafunzo ya vitendo kuhusu matumizi bora ya muda, kufanya maamuzi sahihi na kukuza uwezo binafsi. Kwangu, hiki ni kitabu ambacho ni rafiki wa karibu katika safari ya maisha, kwa kuwa kinampa msomaji uwazi wa fikra, mwelekeo wenye kusudi na nguvu ya kukabiliana na changamoto za maisha.”
Prof. Omari K. Mbura
Profesa wa Masoko na Mkuu wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS).

“Afrika ni bara lenye idadi kubwa ya vijana. Hata hivyo, hatua nyingi za kisera zilizochukuliwa hadi sasa hazijafanikiwa kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya vijana wengi; wanawake kwa wanaume. Ukweli usiopingika ni kwamba, vijana wa Afrika bado wanasalia pembezoni mwa ushiriki wa kisiasa na fursa za kiuchumi. Kutokana na hali hiyo, vijana wengi waliokata tamaa hujikuta wakigeukia njia za vurugu kama suluhisho la changamoto zinazowakabili.
Kitabu hiki kimekuja wakati mwafaka, kikitoa tafakuri za kifalsafa kuhusu nafasi na changamoto za vijana katika jamii ya leo. Jambo la pekee ni kwamba, kinawafundisha na kuwakumbusha vijana namna ya kubadili kipato kuwa utajiri endelevu. Kwa hakika, hiki ni kitabu cha mwongozo wa vitendo kinachowawezesha vijana kujitambua, kukuza uwezo wao na kufikia utimilifu wa maisha yao.”
Dkt. William John Walwa
Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Sasa Ninajua ni kitabu chenye tafakuri nzito, kinachomwelekeza msomaji katika safari ya kujitambua, kugundua kusudi la maisha na kuishi kwa uhalisia. Nguvu kubwa ya kitabu hiki imo katika uwezo wake wa kuifanya falsafa iwe rahisi kueleweka na yenye umuhimu katika maisha ya kila siku. Sura ya Jitambue Mwenyewe ni somo linalopaswa kumfikia kila mtu anayejihisi kupotea katikati ya kelele na misukosuko ya maisha ya kisasa au anayetamani kuelewa kwa kina kusudi la maisha yake. Kwa namna ya pekee, kitabu hiki kinafaa kwa vijana, wataalamu wa fani mbalimbali na watu wote wanaopenda kujifunza katika maisha yao, wanaotafuta uwazi wa fikra katikati ya ulimwengu uliojaa vurugu na vishawishi.
Sasa Ninajua kinakuwa rafiki wa kudumu kwa kila aliye tayari kuandika upya simulizi la maisha yake na kuishi kwa uhalisia. Ninakipendekeza kwa moyo wote kwa kila anayetamani kuitikia wito wa 'Jitambue Mwenyewe' na kujenga maisha yenye maana, kusudi na athari chanya kwa wengine.”
Mchungaji Dkt. Eliona Kimaro
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

“Sasa Ninajua ni kitabu cha falsafa kilichoandikwa na Frateri Aman Lyimo. Kitabu hiki kinawasilisha mawazo ishirini na moja ya kifalsafa kwa ajili ya maisha. Kwa namna ya pekee, mwandishi ameweza kukusanya, kuoanisha na kuendeleza kwa ustadi fikra makini na zenye nguvu kutoka kwa wanafalsafa mashuhuri pamoja na viongozi wanafikra wa Afrika. Kupitia uchambuzi wake wa kina wa kazi zao, ametoa mchango muhimu wenye ujumbe wa msingi, wenye nguvu, unaochochea tafakuri na unaojenga maarifa kwa ajili ya ukuaji wa kifikra katika jamii kwa wanaopenda hekima na wasomaji kwa ujumla.
Ninapendekeza kila mtu akisome kitabu hiki kwa sababu kitamhamasisha na kumwezesha kufikiri kwa kina, kujitegemea na kujenga uwezo wa kujitawala, hasa anapokabiliwa na changamoto, upinzani au ukosoaji usiotarajiwa.”
Bw. Gonsalva Matembo
Mwanafalsafa na Mhadhiri Msaidizi wa Falsafa, Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan, Morogoro, Tanzania.

“Sasa Ninajua: Kutoka Kutokuelewa hadi Uelewa kinatoa mwongozo wa kiakili, kutoka katika hali ya kutokuwa na uhakika hadi kwenye ufahamu na mtazamo mpana wa maisha kupitia falsafa. Kimeandikwa kwa ustadi na kina, ili kutoa mwelekeo sahihi wa kudumu kwa akili inayotafakari na yenye kiu ya kutaka kujua.”
Dkt. Thomas Joseph Nari
Mwanafalsafa na Mhadhiri wa Falsafa, Chuo Kikuu cha Dodoma.
MAONI KWA VIDEO
Falsafa tatu zilizomgusa
Washa sauti.
Namshukuru sana kaka na ndugu yangu Godlisten Malissa, kwanza kwa heshima kubwa ya kushiriki katika uzinduzi wa kitabu changu Sasa Ninajua; zaidi pia kwa kuelezea falsafa tatu zilizomgusa kati ya 21, ambazo angependa vijana tulio wengi kujitahidi kuziishi.
Godlisten Malissa@malisa_gjAlishiriki katika uzinduzi wa Sasa Ninajua.
ASANTE
Siku moja, mhadhiri wetu, Bernadin Mfumbusa, Askofu wa Jimbo Katoliki la Kondoa, alituambia jambo ambalo lilibadili kabisa mtazamo wangu. Alisema,
“Hata hapa Kahama unaweza kusoma Falsafa na kuwa mtu mkubwa. Ukubwa haupatikani kutokana na mahali ulipo, bali hutokana na maono uliyonayo.”
Maneno hayo yaliniguza sana, na nilitoka darasani siku hiyo nikiwa na nguvu mpya. (Soma zaidi Sura ya Nane)
“Bila yeye, na msaada wake wa kupitia na kuhakiki mawazo yangu, nisingeweza kuandika kitabu hiki.”

Askofu Bernadin MfumbusaAlihakiki mawazo yangu na Sura ya Nane, inayohusu maono ndio sababu ya yote. Alifariki Aprili mwaka huu.
Wapi Kukinunua
TZS 25,000/- · kiombe kwa jina lake
Dar es Salaam
Dar es Salaam
Morogoro
Dar es Salaam
Dar es Salaam
Anywhere else
Call or message and I will post it.